Ligi daraja la pili wilaya ya Mjini imeedelea ndani ya uwanja wa Amani kwa kuchezwa mtanange kati ya West coast na Kidongochekundu na mchezo huo kumalizika kwa sare ya bila kufungana.

kikosi cha kidongochekundu baada ya mechi wakiwa na machofu.
Katika mchezo huo kila timu ilikuwa ina hamu ya kutaka kuondoka na ushindi lakini hadi mpira huo ulipomaliza timu hizo ziliweza kugawana alama baada ya kutokufungana.

kikosi cha West coast baada ya mtanange.
West cost imekuwa ikisuasua katika ligi hiyo kwani mpaka sasa wamekuwa na alama nane baada ya mechi hiyo, huku Kdongochekundu wakiwa katika nafasi nzuri ya kutaka kupanda daraja .
|