Home
Sign Up
Log In
Monday
06.23.2025
9:57 AM
Welcome Guest | RSS

            SALMA SPORTS MEDIA


    PATA HABARI MOTOMOTO ZA MICHEZO NDANI NA NJE YA

NCHI. 

                                                                                                                 TANGAZA NASI



WASILIANA NASI KUPITIA +255 779 518 500 / +255 772 997 018 / +255 678 043 812; email: salmahassan040@gmail.com / salminjsalmin@gmail.com



Site menu

Our poll
Rate my site
Total of answers: 3

Statistics

Total online: 1
Guests: 1
Users: 0

  
Home » 2016 » February » 14 » STAND UTD VS SIMBA SC: VIKOSI VINAVYOANZA NA DONDOO MUHIMU
6:44 PM
STAND UTD VS SIMBA SC: VIKOSI VINAVYOANZA NA DONDOO MUHIMU

Michezo mitano inapigwa leo kwenye ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara, macho na masikio ya wengi ni kwenye mchezo wa Stand United vs Simba SC kwenye uwanja wa CCM Kambarage mkoani Shinyanga.

Kwanini Stand United vs Simba ni mechi inayozungumzwa sana?

Mchezo huu unapewa uzito mkubwa kwasababu endapo Simba wakishinda mchezo huu basi watafikisha pointi 45 na kukaa kileleni mwa ligi japo kwa muda wakisubiri matokeo ya kesho ya mechi ya Coastal Union vs Azam FC. Azam na Simba zinalingana pointi lakini Simba wana wastani mzuri wa magoli ya kufunga na kufungwa, baada ya kucheza mechi 18 Simba imefunga magoli 33 huku ikiwa imeruhusu magoli na tofauti ni magoli 23 wakati Azam wamefunga magoli 31 na kufungwa magoli 10 kwenye michezo 16 waliyocheza na kufanya wawe na tofauti ya magoli 21 hivyo kuzidiwa kwa magoli 2 na Simba.

Simba haijawahi kukaa kileleni kwa misimu mitatu sasa, na ushindi kwenye mchezo wa leo ndiyo fursa pekee kwao kukaa kileleni baada ya kusubiri kwa misimu mitatu mfululizo.

Endapon Stand United itashinda mchezo huu itafikisha jumla ya pointi 32 itabakia nafasi ya tano nyuma ya Mtibwa Sugar yenye pointi 33.

Timu hizi zimeshakutana mara tatu kwenye mechi za ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara, katika michezo hiyo Simba imeshinda mchezo mmoja na Stand United imeshinda mchezo mmoja huku zikitoka sare kwenye mchezo wao mmoja.

Head to head Stand United vs Simba SC

October 4, 2014 Simba 1-1 Stand United

February 22, 2015 Stand United 1-0 Simba

September 30, 2015 Simba 1-0 Stand United

Wafungaji wenye magoli mengi kwa timu zote

Stand United: Elias Maguri- magoli 9

Simba SC: Hamisi Kiiza- magoli 14

Nafasi zilipo timu zotembili kwenye msimamo wa ligi

Simba SC: nafasi ya pili, pointi 42

Stand United: nafasi ya tano, pointi 29

Uwanja: CCM Kambarage-Shinyanga

Kikosi cha Stand United kitachoanza: Frank Muwonge, Revocatus Richard, Seleman Mrisho, Nassor Masoud, David Osman, Jacob Masawe, Pastory Athanas, Amri Kiemba, Elias Maguri, Seleman Selembe.

Subs: Mohamed Makaka, Frank Hamis, Jeremia Enock, Jeremia Katura, Hasan Sefu, Aron Lulambo, Erick Kayombo.

Kikosi cha Simba SC kitakochoanza: Vicent Agban, Emiry Nimuboma, Hassan Kesy, Hassan Banda, Juuko Murshidi, Justice Majabvi, Mwinyi Kazimoto, Jonas Mkude, Hamisi Kiiza, Ibrahim Ajib, Said Ndemla-13

Subs: Peter Manyika, Novaty Lufunga, Hassan Isihaka, Awadh Juma, Brian Majwega, Daniel Lyanga, Mussa Mgosi.

Waamuzi wa mchezo:

Ludovick Charles-Kagera

Line one: Grace Wamara-Kagera

Line two: Jopseph Masija-Mwanza

Fourth Official: Jimmy Fanuel-Shinyanga

Chanzo: Shaffih Dauda

Views: 245 | Added by: salminjsalmin | Rating: 0.0/0
Total comments: 0
avatar

Visitors
idadi ya watembeleaji
Idadi ya watembeleaji

WATEMBELEAJI

Entries archive

Salma Sport Media © 2025
uCoz