Home
Sign Up
Log In
Monday
06.23.2025
10:56 AM
Welcome Guest | RSS

            SALMA SPORTS MEDIA


    PATA HABARI MOTOMOTO ZA MICHEZO NDANI NA NJE YA

NCHI. 

                                                                                                                 TANGAZA NASI



WASILIANA NASI KUPITIA +255 779 518 500 / +255 772 997 018 / +255 678 043 812; email: salmahassan040@gmail.com / salminjsalmin@gmail.com



Site menu

Our poll
Rate my site
Total of answers: 3

Statistics

Total online: 2
Guests: 2
Users: 0

  
Home » 2016 » February » 14 » SABABU 5 ZA SIMBA KUSHINDA DHIDI YA STAND UNITED
7:54 PM
SABABU 5 ZA SIMBA KUSHINDA DHIDI YA STAND UNITED

 

Simba jana ilipata ushindi wake wa pi mbele ya Stand United ya mkoani Shinyanga kwenye pambano ambalo lilipigwa Kambarage. Ushindi huo ulikuwa ni wa pili kati ya mara nne ambazo timu hizo zimekutana kwenye michezo ya ligi tangu Stand ipande daraja msimu uliopita.

Baada ya kuangalilia kwa makini mchezo huo kati ya timu hizo mbili, shaffihdauda.co.tz imegundua kwamba Simba ilikuwa inachagizwa na vitu vingi kuibuka na ushindi kwenye mchezo huo ukilinganisha na wapinzani wao ambao walikuwa ni Stand United.

Hizi ni sababu tano ambazo kwa kiasi kikubwa sana zilichangia ushindi wa Simba kwenye mchezo wa jana

Historia

Simba na Stand United zilikuwa zimekutana kwenye michezo mitatu ya ligi kuu Tanzania bara kabla ya mchezo wa jana ambao Simba ilishinda kwa bao 2-1 kwenye uwanja wa CCM Kambarage Shinyanga.

Katika michezo hiyo mitatu Simba ilikuwa imeshinda mchezo mmoja kwenye uwanja wa taifa na Stand United pia ilikuwa imeshinda mchezo mmoja kwenye uwanja wa Kambarage huku timu hizo zikitoka sare kwenye mchezo mmoja kwenye uwanja wa taifa.

October 4, 2014 Simba 1-1 Stand United

February 22, 2015 Stand United 1-0 Simba

September 30, 2015 Simba 1-0 Stand United

Matokeo hayo yaliifanya Simba kuingia kwenye mchezo huo kwa nguvu zote wakijua lolote linaweza kutokea kwasababu Stand United wamekuwa hawatabiliki kwasababu Simba hata ilipofanikiwa kupata ushindi dhidi ya Stand basi umekuwa ni ushindi wa magoli machache.

Morali ya ushindi

Simba iliingia kwenye mchezo dhidi ya Stand ikiwa na kumbukumbu ya kushinda mechi tano za ligi na moja ya FA chini ya kocha wao Jackson Mayanja.

Matokeo hayo yaliwajengea wachezaji wa Simba hali ya kujiamini wakati wanaingia uwanjani kukabiliana na Stand na hilo lilichangia kwa kiasi kikubwa timu yao kupata ushindi kwenye mchezo wa jana.

Kukaa kileleni mwa ligi

Wachezaji, bechi la ufundi, viongozi na mashabiki wa ‘myama’ walikuwa wakitambua fika ushindi wa mechi dhidi ya Stand ungewapa fursa ya kuongoza ligi japo kwa muda wakati wakisubiri kuona mechi nyingine zinachezwa.

Kigezo cha kuongoza ligi kiliwapa wachezaji nguvu ya kujituma zaidi kutaka kushinda mchezo huo, jambo hilo lilifanikiwa na Simba kwa mara ya kwanza iliongoza ligi jana baada ya ushindi wa magoli 2-1 dhidi ya Stand United. Mara ya mwisho Simba kukaa kileleni mwa ligi ilikuwa ni mwanzoni mwa msimu wa mwaka 2013-14.

Kocha, Viongozi na Mashabiki

Jackson Mayanja tangu ameichukua Simba ameiongoza kupata ushindi mfululizo jambo hilo limewafanya viongozi na mashabiki kumuamini na kumsahau kabisa mwingereza Dylan Kerr. Uongozi, wachezai  na wanachama Simba wamekuwa kitu kimoja na hali ilivyo kwasasa inaonekana ni shwari na hakuna mgawanyiko ndani ya Msimbazi.

Mechi ijayo ya Simba

Mechi ijayo Simba itakutana na Yanga kwenye uwanja wa taifa, Simba ilihitaji matokeo mazuri ambayo hayatawaumiza wakati huu wanapowania ubingwa wa bara bali matokeo ambayo yatawafanya wajiamini ukizingatia walipoteza mchezo wa kwanza dhidi ya watani zao.

chanzo:shaffih dauda.

Views: 224 | Added by: salminjsalmin | Rating: 0.0/0
Total comments: 0
avatar

Visitors
idadi ya watembeleaji
Idadi ya watembeleaji

WATEMBELEAJI

Entries archive

Salma Sport Media © 2025
uCoz