Home
Sign Up
Log In
Monday
06.23.2025
9:31 AM
Welcome Guest | RSS

            SALMA SPORTS MEDIA


    PATA HABARI MOTOMOTO ZA MICHEZO NDANI NA NJE YA

NCHI. 

                                                                                                                 TANGAZA NASI



WASILIANA NASI KUPITIA +255 779 518 500 / +255 772 997 018 / +255 678 043 812; email: salmahassan040@gmail.com / salminjsalmin@gmail.com



Site menu

Our poll
Rate my site
Total of answers: 3

Statistics

Total online: 1
Guests: 1
Users: 0

  
Home » 2016 » February » 15 » Sababu 4 Kwanini Real Madrid Hawataki Fainali ya Copa Ichezwe Bernabeu
5:04 PM
Sababu 4 Kwanini Real Madrid Hawataki Fainali ya Copa Ichezwe Bernabeu

The Santiago Bernabeu limeshakuwa mwenyeji wa fainali za kombe la Copa Del Rey mara 13 tangu mwaka 1976-77, wakati lilipobafilishwa jina kutoka kuwa Copa del Generalisimo, fainali 4 kati ya hizo zilifanyika chininya utawala wa Florentino Perez.


Hakuna fainali hata moja kati ya hizo 4 chini ya Perez ambayo iliihusisha Barcelona. Fainali mbili kati hizo ziliihusisha Real Madrid na zilizobaki zilihusisha timu za Zaragoza, Osasuna, Betis na Espanyol. Chama cha soka cha Spain na baadhi ya wadau wanataka fainali ya msimu huu ifanyike Santiago Bernabeu lakini Real Madrid, wamiliki wa kiwanja hicho hawapo tayari kuruhusu jambo hilo na hizi zifuatazo ni sababu 4 juu ya kugoma kwao.

Sababu mbili za kwanza
Fainali mbili za Copa del Rey zilizofanyika Barnabeu huku Madrid wakicheza kwenye fainali hizo, ziliisha kwa kipigo. Walipoteza fainali ya kwanza dhidi ya Deportivo kwa kufungwa 2-1, mchezo ambao ulichezwa siku ambayo walikuwa wanatimiza miaka 100 tangu kuanzishwa kwa klabu hiyo.

Fainali ya pili walipoteza dhidi ya Atletico Madrid, 2-1 katika muda wa nyongeza. Baada ya fainali hizo, Florentino Perez akaamua kufunga milango kwa fainali za kombe hilo kufanyika Santiago Bernabeu.

Sababu ya tatu
Inawezekana hii ikawa sababu kuu kabisa kwanini Madrid hawataki fainali ya Copa De Rey ifanyike uwanjani kwao. Kumbukumbu mbaya zaidi waliyonayo Madrid ni ile ya msimu wa fainali ya 1996-97, ambayo Barcelona walicheza dhidi Real Betis. Huku timu yao ikiundwa Figo, Baia, Luis Enrique na Amunike, Barcelona wakamaliza mechi kwenye muda wa ziada na ushindi. Raisi wa wakati huo Joan Gaspart akafanikiwa kuwezesha wimbo wa BArcelona ukachezwa kwenye music system ya uwanja wa Santiago Bernabeu, kitendo hicho kilikuwa kama kuchoma kisu kwenye moyo wa kila shabiki wa Madrid. Tangu wakati huo, Barcelona hawajawahi kucheza fainali katika dimba hilo.

 Sababu ya 4
Madrid bado wamekasirishwa na kitendo cha kuondokewa kwenye michuano hiyo kwasababu ya kesi ya kumchezesha Cheryshev. Hawakupenda namna kesi yao ilivyamuliwa.

Views: 149 | Added by: salminjsalmin | Rating: 0.0/0
Total comments: 0
avatar

Visitors
idadi ya watembeleaji
Idadi ya watembeleaji

WATEMBELEAJI

Entries archive

Salma Sport Media © 2025
uCoz