Home
Sign Up
Log In
Monday
06.23.2025
10:05 AM
Welcome Guest | RSS

            SALMA SPORTS MEDIA


    PATA HABARI MOTOMOTO ZA MICHEZO NDANI NA NJE YA

NCHI. 

                                                                                                                 TANGAZA NASI



WASILIANA NASI KUPITIA +255 779 518 500 / +255 772 997 018 / +255 678 043 812; email: salmahassan040@gmail.com / salminjsalmin@gmail.com



Site menu

Our poll
Rate my site
Total of answers: 3

Statistics

Total online: 2
Guests: 2
Users: 0

  
Home » 2016 » February » 14 » NI VYEMA KUYAJUA HAYA KABLA YA MECHI YA MAN CITY VS SPURS
7:57 PM
NI VYEMA KUYAJUA HAYA KABLA YA MECHI YA MAN CITY VS SPURS

 

Kwa upande wa Manchester City nahodha wao Vincent Kompany amepona na yuko tayari kwa mchezo wa leo. Kompany alikuwa akiuguza majeraha yake tangu Boxing Day alipopata majeraha ya nyama za nyuma ya ugoko.

David Silva naye yuko fiti tayari kwa mchezo wa leo lakini Fabian Delph atakuwa nje kwa wiki saba kutokana na kusumbuliwa na majeraha na Bacary Sagna hatakuwepo kutokana na kusumbuliwa na jeraha la goti.

Kwa upande wa Tottenham, kiungo wao maridadi kinda Dele Alli anataraji kuwepo baada ya kuingia akitokea benchi wikiendi iliyopita.

Kevin Wimmer na Jan Vertonghen wataendelea kuwa nje kutokana kutopona majeraha yao.

Mameneja wanasemaje?

Meneja wa Manchester City Manuel Pellegrini: “Kama nilivyosema wiki iliyopita, sio mchezo wenye kutoa maamuzi lakini wenye umuhimu mkubwa sana  Ni muhimu sana kujaribu kurudi kileleni mwa ligi. Timu mbili ama tatu hivi zipo juu yetu kwa wakati huu, hivyo ni lazima tujaribu kurudi katika mbio za ubingwa mapema iwezekanavyo.

“Vincent Kompany amekuwa akijiweka fiti kwa takriban wiki tatu sasa. Amecheza kwa dakika 45 katika mchezo wa kirafiki kwenye timu ya vijana chini ya umri wa miaka 21 na nadhani kwa sasa yuko kamili kabisa.”

Kocha wa Tottenham Mauricio Pochettino: “Ili kufika mbele zaidi au kuongeza wigo kwenye nafasi tuliyopo, ni lazima tupate ushindi katika michezo yetu.

“Lakini huu sio mchezo wenye kutoa maamuzi. Ni muhimu sana lakini sio mchezo wa mwisho wa ligi.

“Wanafahamu na tunafahamu pia, tuko katika nafasi ambayo tunahitaji michezo 13 mbele, lakini baaada ya mchezo huu tunabaki na michezo 12 na sasa tunaingia katika kipindi ambacho ni muhimu zaidi katika ligi.”

Takwimu za mchezo (Head-to-head)

  • Manchester City wamewafunga Tottenham katika michezo yote walicheza wakiwa katika dimba la Etihad.
  • Wamefunga magoli 10 katika michezo yao miwili ya mwisho dhidi ya Spurs kwenye dimba la Etihad, wakishinda 6-0 na 4-1.
  • Ushindi wa magoli 4-1 wa Spurs katika raundi ya kwanza ulikuwa ni ni ushindi wao wa pili ndani ya michezo 11 katika ligi dhidi ya (Wameshinda 2, Droo1, kufungwa 8).
  • Katika michezo tisa iliyopita, yamepatikana magoli 41- ukiwa ni wastani wa magoli 4.5 kwa mchezo.

Manchester City

  • Vijana wa Manuel Pelligrini wameshinda pointi 21 katika michezo yao 9 ya kwanza lakini wamejikusanyia pointi 26 kutoka kwenye michezo 16.
  • Walikuwa nyuma kwa alama 11 dhidi ya Leicester na pointi nane nyuma ya Tottenham wakati kila timu ilipokuwa imecheza michezo16.
  • Manchester City wamepoteza mchezo mmoja tu katika michezo yote ambayo wao ndiyo walianza kupata goli, wameshinda 14, wamepoteza mmoja
  • Ikiwa watafungwa mchezo wa leo, basi itakuwa ni mara yao ya kwanza kupoteza mechi bili mfululizo nyumbani tangu Desemba 2008.
  • Sergio Aguero amefunga magoli 10 ndani ya michezo nane ambayo amecheza dhidi ya Tottenham. Kwa mwaka huu wa 2016, yeye ndio anaingoza kwa kufunga magoli mengi, akiwa amefunga magoli saba.

Tottenham

  • Tottenham wameshinda michezo minne mfululizo, takwimu bora kwa sasa kunako ligi kuu ya England.
  • Wana rekodi nzuri sana ya safu ya ulinzi, wameruhusu magoli 19.
  • Hakuna timuyoyote ambayo ina rekodi nzuri ya kutokea nyuma na kushinda mchezo kama Spurs msimu huu, wamefanya hivyo katika michezo 14 msimu huu.
  • Dele Alli maefunga magoli 11 ndani ya michezo 14 aliyocheza msimu huu (magoli sita, pasi za magoli tano).
  • Harry Kane amefunga magoli 14 katika michezo yake ya mwisho 16 ya Ligi Kuu Engalnd. appearances.
Views: 196 | Added by: salminjsalmin | Rating: 0.0/0
Total comments: 0
avatar

Visitors
idadi ya watembeleaji
Idadi ya watembeleaji

WATEMBELEAJI

Entries archive

Salma Sport Media © 2025
uCoz