Home » 2016»February»16 » Neymar alalamika Suarez kamuibia penati ya Messi.
8:17 AM
Neymar alalamika Suarez kamuibia penati ya Messi.
Moja ya story kubwa sasa hivi kwenye soka ni kuhusu penati ya Messi kwenye mechi dhdi ya Celta Vigo. Penati ile ambayo Messi amempasia mpira na Suarez akafunga inasemekana ilikua ni ya Suarez.
Kwenye video inaonyesha jinsi Neymar alivyoenda kuiomba kwa Messi mara baada ya kukwatuliwa. Baada ya kupiga ile pasi, Suarez akatoka mbio na kwenda kufuga goli.
Baada ya kushangilia Neymar alionekana akimlaumu Suarez kwamba ameiba penati yake wakati yeye ndiye ilibidi aipige.
Messi na Suarez walionekana kumcheka Neymar akilalamika na Suarez akijitahidi kujitetea baada ya kuipiga.