Muhammed Cisso ni mchezaji anaevalia jezi nambari sita mgongoni (6) katika timu ya Kwaalinato United na anacheza nambari tano (5) uwanjani.
Katika uchezaji wake kijana Cisso wachezaji wenzake na mashabiki mbalimbali wanamtambua kwa sifa yake kuu ya uhodari katika umiliki wa mpira na kucheza sana mipira ya kichwa, ni mara nyingi anajiandikia magoli yake kupitia ufundi wa kupiga kichwa.

Katika mazungumzo baina yangu na mchezaji huyu, alionesha moyo mkubwa sana wa mafanikio aliyojipangia ikiwa ni pamoja na hakikisha kipaji chake kinazidi kukua na kufanikiwa kucheza katika timu kubwa ndani na nje ya nchi.
Kadhalika sikuacha kumuuliza juu ya mtazamo wake wa soka la zenj kwa ujumla nauonaje, majibu yake yalikua “zanzibar kuna vipaji na vinaongezeka ila tatizo ni moja tu, hakuna watu wa kudhamini katika soka letu la zenji yaani hiyo ndio changamoto kubwa iliyoikumba zenj katika mpira wa miguu ni wawezeshaji tu hakuna, si unaona mwenye na unashuhudia vipaji vyetu lakini unafikiri nani atuone, wote wanaishia kwengineko uko lakini sisi baadae tunaishia mitaani, na kama leo tu wanajitokeza zenj itakua kuliko unavyofikiria”alisema Cisso.
Hapohapo nilimbandika suala jengi “unafikiri ni kwanini wadhamini hawajitokezi” jibu lake ilikua ni “Z.F.A nahisi hawajawa tayari”.
Pia amesema iwapo wadhamini watajitokeza kudhamini ligi na wachezaji kufika mpaka mitaani ndani na kuwaona basi soka la zenji litakuwa kama ligi kuu ya Vodacom VPL.
Cisso ni mchezaji mwenye umri wa miaka ishirini na moja (21) ni hodari sana hata SALMA SPORTS MEDIA ilimshuhudia akionesha makeke yake uwanjani, ni mzuri katika kumiliki mpira, makini katika maamuzi na vicchwa katika krosi apo ndipo utakapo ufaidi ufundi wake.
Laiti kama watawezeshwa wachezaji kama hawa bila ya shaka na huu ndio ukweli usiopingika Cisso atakua ni mmoja kati ya wachezaji wenye kupigiwa mfano Tanzania ukweli anakipaji cha sifa lakini ikowapi ZFA wakuvionesha vijapi hivyo.
Kwa mawasiliano na Cisso ni kupitia +255 774 543 596