Home
Sign Up
Log In
Monday
06.23.2025
12:08 PM
Welcome Guest | RSS

            SALMA SPORTS MEDIA


    PATA HABARI MOTOMOTO ZA MICHEZO NDANI NA NJE YA

NCHI. 

                                                                                                                 TANGAZA NASI



WASILIANA NASI KUPITIA +255 779 518 500 / +255 772 997 018 / +255 678 043 812; email: salmahassan040@gmail.com / salminjsalmin@gmail.com



Site menu

Our poll
Rate my site
Total of answers: 3

Statistics

Total online: 1
Guests: 1
Users: 0

  
Home » 2016 » February » 18 » MIEMBENI CITY YAZIDI KUJIKITA KILELENI.
7:55 AM
MIEMBENI CITY YAZIDI KUJIKITA KILELENI.

 

Kilabu ya Miembeni City inayoshiriki ligi soka daraja la pili taifa Unguja imezidi kujikita kileleni mwa kundi A ligi soka daraja la pili taifa Unguja baada yakuifunga timu ya FC Lion jumla ya magol 3-1 ikiwa ni muendelezo wa ligi hiyo mchezo ulichezwa katika kiwanja cha Amani hapo jana mnamo majira ya saa 8 mchana.

City imejikita kileleni mwa kundi A ikiwa na alama 30  baada yakucheza michezo 12 ya mzunguko wa kwanza bila yakupoteza mchezo hata mmoja ikiwa imeshinda michezo tisa tisa 9 nakutoka sare michezo mitatu.

 

Akizungumzia mafanikio ya klabu hiyo msemaji wa klabu hiyo Ally Khamis Ibny amesema mafanikio hayo yanatoka na ari iliyopo kwa wachezaji sambamba na masharikiano ya viongozi wa klabu pamoja na mwalimu wa timu.

“Unajua huwezi kuwa na mafanikio katika jambo lolote lile bila yakuwepo kwa mashirikiano hivyo wachezaji wetu viongozi pamoja na mwalimu wote wapo kitu kimoja ili kuhakikisha timu inapata matokeo mazuri katika kila mchezo”Alisema Ibny.

 

Aidha amaeongeza kuwa aina ya wachezaji ambao wanasajili katika kikosi chao pia ni chachu ya ushindi nakuongeza kuwa wanatoa kipaombele zaidi kwa vijana.

 

Akizungumzia mzunguko wa pili wa ligi msemaji huyo amesema anajua utakuwa na michezo migumu huku akiamini kuwa kila timu itakuwa na hamu yakutufunga hivyo watahakikisha wanajiandaa vyakutosha ili kuendeleza heshima yakutokupoteza, ambayo wameianza tokea msimu uliopita.

 

“Mzunguko wa pili utakuwa mgumu sana najua kila timu itataka itufunge hivyo tutahakikisha tunajipanga vyakutosha ili kufanya vyema katika kila mchezo ili kuendeleza rekodi yetu yakutokupoteza katika mzunguko huo ambao tunangoja ratiba itoke tu” Aliongeza Ibny.

 

Miembeni City ambayo haijawahi kupoteza mchezo hata mmoja wa ligi kwa misimu miwili sasa ambapo katika msimu wa 2014-2015 imeshiriki ligi daraja la pili wilaya ya mjini bila yakupoteza mchezo hata mmoja hadi kupandisha timu daraja na katika msimu wa 2015-2016 mpaka sasa imeshacheza michezo 12 bila yakupoteza mchezo hata mmoja.

Views: 208 | Added by: salminjsalmin | Rating: 0.0/0
Total comments: 0
avatar

Visitors
idadi ya watembeleaji
Idadi ya watembeleaji

WATEMBELEAJI

Entries archive

Salma Sport Media © 2025
uCoz