Home
Sign Up
Log In
Monday
06.23.2025
2:31 PM
Welcome Guest | RSS

            SALMA SPORTS MEDIA


    PATA HABARI MOTOMOTO ZA MICHEZO NDANI NA NJE YA

NCHI. 

                                                                                                                 TANGAZA NASI



WASILIANA NASI KUPITIA +255 779 518 500 / +255 772 997 018 / +255 678 043 812; email: salmahassan040@gmail.com / salminjsalmin@gmail.com



Site menu

Our poll
Rate my site
Total of answers: 3

Statistics

Total online: 1
Guests: 1
Users: 0

  
Home » 2016 » February » 15 » Michezo isivunje maadili.
8:15 AM
Michezo isivunje maadili.

 

Walimu wa Michezo katika Wilaya ya Micheweni wametakiwa kuandaa michezo yenye kwendana na maadili na utamaduni wa mzanzibar .

 

Kauli hiyo imetolewa na Afisa Elimu na Mafunzo ya Amali Wilaya ya Micheweni mwl Mbwana Shame Said wakati akizungumza na walimu hao kwenye kituo cha uwalimu Wingwi .

 

Amesema kwamba ni vyema walimu wanapoandaa michezo kwa ajili ya elimu bila ya malipo wanatakiwa kuzingatia sana maadili ili kusiwepo na upotoshwaji wa tamasha hilo .

 

Aidha amewataka walimu kutambua dhamana zao jambo ambalo litasaidia kudumisha nidhamu kwa wanafunzi .

 

Naye Afisa Michezo na Utamaduni Wilaya hiyo amewataka walimu hao kuanza maadalizi mapema kwa kuangazlia vipengele muhumi ambavyo vinaweza kusaidia skuli zao kupata ushindi .

 

Kikao hicho ni maandalizi ya Tamasha la Elimu bila ya malipo ambalo kwa Pemba linatarajia kuzinduliwa tarehe 13 mwezi huu katika wilaya ya chake chake.

Views: 140 | Added by: salminjsalmin | Rating: 0.0/0
Total comments: 0
avatar

Visitors
idadi ya watembeleaji
Idadi ya watembeleaji

WATEMBELEAJI

Entries archive

Salma Sport Media © 2025
uCoz