Home
Sign Up
Log In
Monday
06.23.2025
11:53 PM
Welcome Guest | RSS

            SALMA SPORTS MEDIA


    PATA HABARI MOTOMOTO ZA MICHEZO NDANI NA NJE YA

NCHI. 

                                                                                                                 TANGAZA NASI



WASILIANA NASI KUPITIA +255 779 518 500 / +255 772 997 018 / +255 678 043 812; email: salmahassan040@gmail.com / salminjsalmin@gmail.com



Site menu

Our poll
Rate my site
Total of answers: 3

Statistics

Total online: 1
Guests: 1
Users: 0

  
Home » 2016 » February » 19 » Man Utd walazwa Denmark Europa League
7:54 AM
Man Utd walazwa Denmark Europa League

 

Manchester United walijikwaa katika juhudi zao za kufana Ulaya baada ya kushindwa ugenini na klabu ndogo kutoka Denmark katika Europa League....


United walichapwa mabao 2-1 na timu ndogo ya Midtjylland.

Klabu hiyo ya Old Trafford pia ilipata pigo baada ya kipa wake namba moja David de Gea kuumia kifundo cha mguu wakati akipasha mwili moto na nafasi yake kuchukuliwa na Kipa wa Argentina Sergio Romero.

 

Man Utd walitangulia kufunga kupitia Memphis Depay lakini Midtylland wakasawazisha kupitia Pione Sisto na Paul Onuachu alifunga bao la ushindi.

Manchester United walishindwa na Sunderland 2-1 Jumamosi Ligi ya Premia na wamepungukiwa na alama sita kufikia nambari nne, nafasi ya kufuzu Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya.

Meneja wao Louis van Gaal majuzi alisema kushinda Europa League ndio njia rahisi kwao kufuzu kwa ligi hiyo ya mabingwa Ulaya msimu ujao.

Kwenye mechi nyingine zilizochezwa Alhamisi usiku, Borrusia Dotmund wakicheza katika uwanja wao wa nyumbani, walipata ushindi wa 2-0 dhidi ya FC Porto

Matokeo mengine ni:
Tottenham 1-1 Fiorentina
Valencia 6-0 Rapid Vienna.
Liverpool 0-0 Augsburg.
Anderlecht 1 –0 Olympiakos
Sevilla 3- 0 Molde
St Etienne 3-2 Basel
Villarreal 1- 0 Napoli
FC Sion 1-2 Sporting Braga
Galatasaray 1-1 Lazio
Marseille 0-1 Ath Bilbao

Views: 200 | Added by: salminjsalmin | Rating: 0.0/0
Total comments: 0
avatar

Visitors
idadi ya watembeleaji
Idadi ya watembeleaji

WATEMBELEAJI

Entries archive

Salma Sport Media © 2025
uCoz