Ligi kuu ya Zanzibar kanda ya Unguja itaendelea leo hii kwa kuanzwa kuchezwa mchezo wa mzunguko wa pili kati ya timu ya KVZ na Mtende, mchezo ambao utachezwa majira ya saa kumi 10:00 za jioni ndani ya dimba la Amani mjini Zanzibar.

Mchezo huo utakuwa ni wa raundi ya kumi na sita (16) ambapo KVZ wataingia uwanjani wakiwa nafasi ya sita (6) na alama ishirini 20,huku wakiwa wameshacheza michezo kumi na tatu (13), wameshinda michezo sita (6), wamepoteza michezo mitano (5) na sare michezo miwili (2).
Wakati wapinzani wao Mtende wakiwa ndio wanaoshika mkia wakiwa na alama sita(6), ambao wamecheza michezo kumi na tatu (13),wameshinda mchezo mmoja, wamefungwa michezo tisa (9) na wametoka sare michezo mitatu(3) katika ligi hiyo.
Je? Mdau wa soka wewe karata yako unaitupia wapi katika mchezo huu wa leo?
|