Timu ya KVZ, imeanza vyema katika mzunguko wake wa pili baada ya kuicharaza Mtende mabao 2-0 katika mchezo wa ligi kuu ya Zanzibar kanda ya Unguja uliosukumwa jana jioni ndani ya dimba la Amani mjini Zanzibar.

Katika mchezo huo mchezaji Abdillah Seif Bausi alianza kuipatia KVZ bao la kwanza ndani ya dakika ya 26 baada ya kuupiga mpira wa adhabu nje ya 18 iliyotokana na mchezaji wa Mtende Ali Mwinyi kumfanyia madhambi mchezaji wa KVZ Abbas Abdallah, na bao la pili liliwekwa kimyani na mchezaji Emill Willium mnamo dakika ya 58 ya mchezo huo.

KVZ waliwahi kukutana na Mtende katika mzunguko wa mwano na KVZ waliibuka na ushindi wa bao moja kwa bila dhidi ya Mtende.
Kwa matokeo hayo timu ya KVZ imepanda hadi nafasi ya tatu 3 wakiwa na alama 23, huku Mtende wakiendelea kuburura mkia wakiwa na alama sita.
|