Home
Sign Up
Log In
Monday
06.23.2025
10:58 AM
Welcome Guest | RSS

            SALMA SPORTS MEDIA


    PATA HABARI MOTOMOTO ZA MICHEZO NDANI NA NJE YA

NCHI. 

                                                                                                                 TANGAZA NASI



WASILIANA NASI KUPITIA +255 779 518 500 / +255 772 997 018 / +255 678 043 812; email: salmahassan040@gmail.com / salminjsalmin@gmail.com



Site menu

Our poll
Rate my site
Total of answers: 3

Statistics

Total online: 3
Guests: 3
Users: 0

  
Home » 2016 » February » 21 » KUNA VIPAJI WALA HAVITUNZWI BAADAE TWALALAMA.
1:27 PM
KUNA VIPAJI WALA HAVITUNZWI BAADAE TWALALAMA.
 
Mpenzi msomaji wa makala hii fupi, napenda ufahamu kuwa Zanzibar ni nchi iliyojaaliwa neema ya kila namna hapa ndio kwao.
 
Katika pishapisha zangu mitaani kwa lengo la kufanya utafiti kwa kile kinachaelezwa na watu wengi sana kua nchii hii inavipaji vingi sana lakini havionekani na baadae huishia mitaani na kusahaulika na kwa upande mwengine kua nchii hii inawataalamu wengi lakini hawajaliwi na kuthamiwa mwishoe hutoweka na kwenda kwenye tija zaidi na kupawacha nyumbani pakiwa patupu vumbi tupu kila siku hakuna kijuulikanacho.
 
Unaweza wa kujiuliza kwanini wameondoka lakini pia unaweza kujiuliza kwanini wabakie, hapa nazungumzia wataalamu na makocha wa mpira wa miguu ukiachilia mbali wachezaji ambao bado wapo katika vikona vya viwanja wakijisakatia kabumbu kama starehe ya nafisi.
 
Katika Makala haya tumtazame mtu kama Hababuu Ali Omar (Kocha Hababuu) ni kocha aliekocha kwa ufundishaji,wadau wa soka wote waonapo jina hili basi wanatambua ni upi umahiri kwa kocha Hababuu.
 
Huyu ni mzanzibar halisi aliezaliwa 20 may 1977 katika hospitali kuu Mnazi Mmoja Zanzibar, amesoma Zanzibar na amekulia Zanzibar .
 
Ameanza harakati za kufundisha soka tangia 1996 katika timu ya Junior iitwayo Napoli ya Muembe Makumbi, mpaka 2000 kutoka 2001-2004 aliifundisha timu ya Amaan Fresh,tokea 2004-2006 Gold Fighters ya Kibandamaiti.
 
Si hapo tu 2007 aliifundisha timu ya Black Sailors, 2008- 2009 Gold Fighters kwa mara nyengine tena tena, kutoka 2009-2011 Mwera Stars, 2011-2014 Viko Phamacy pia 2015 aliifundisha timu Malindi.
 
Kadhalika pia aliwahi kufundisha timu za taifa na Combaine , 2002 Combaine ya Wilaya ya Mjini, lakini nyuma kidogo mmna mwaka wa 1997 aliwahi kufundisha timu katika Skuli ya Haile Sellassie,tukiendelea tena 2005-2006 pia aliifundisha timu kutoka chuo cha suza Suza.
 
Pasipo na shaka yoyote ni lazima huyu tumwite hodari mote humo alimo pitia aliwacha athari ya wema na kufanya vyema katika michuano mbalimbali,shujaa huyo hakuishia hapo 2009 alifundisha timu ya taifa ya vijana under 20 akiwa kama Assistance Coach, 2014 alikua kocha mkuu wa timu ya taifa ya Tanzania ya Serengeti Boys Under 17.
 
Hii ni lulu kutoka Zanzibar lakini muda huu ing’aa hukoo, mana kwa sasa yupo Sunderland Academy na kufika kwake huko baada ya kukuta na “Stewart” kocha wa Azam na kuona ujuzi wake na kipaji chake katika ufundishaji hatimae alimpeleka “JMK PARK”.
 
Katika timu zote izo alizopita hakuna alielalama kutokana na ufundishaji wake zaidi ya kusifia juu ya mafanikio waliyoyapata mfano wa hayo na yasioweza kubishaniwa ni pale alipoitoa timu ya Amani Fresh daraja la pili mpaka ligi kuu,si hayo tu yapo mengine mengi.
 
Suala la kujiuliza ni kwanini vipaji kama hivi vinashindwa kenziwa na kulindwa kwa hali yoyote ile na badala yake kuacha tu bila ya kuthaminiwa wala kuonekana kwa wanalolifanya,leo hii tungekua nae Zanzibar yeye na wenzake kama hawa unafikiri ni kwa kiwango gani Zanzibar ingekua juu kisoka?
 
Unafikiri kwa mtindo huu kweli wazanzibar tuta ng'ara katika giza hili lililotuandana ikiwa nyota twazifunikwa kwa mikono yetu wenue.
Views: 316 | Added by: salminjsalmin | Rating: 0.0/0
Total comments: 0
avatar

Visitors
idadi ya watembeleaji
Idadi ya watembeleaji

WATEMBELEAJI

Entries archive

Salma Sport Media © 2025
uCoz