Mkali wa mpira wa kikapu kutoka Marekani Kobe Bryant, alicheza mechi yake ya NBA All Star kwa mara mwisho iliyoandaliwa mjini Toronto nchini Canada.

Nyota wa Los Angeles Lakers Kobe Bryant apewa heshima kubwa wakati wa mechi yake ya mwisho ya NBA All Star
Kobe Bryant alipewa heshima kubwa ya kuagwa na jumuiya ya NBA baada ya kutangaza mpango wa kustaafu uchezaji mwishoni mwa msimu huu.
Kobe Bryant mwenye umri wa miaka 37, alipewa heshima kubwa na wapenzi wa mpira wa kikapu dakika chache kabla ya mechi ya NBA All Star kumalizika.
Kobe Bryant ambaye amecheza katika ligi ya NBA kwa misimu 20, alisambaza picha na video za NBA All Star akiwa na wachezaji wenzake kwenye mitandao ya jamii na kuweza kufikia mashabiki zaidi ya milioni 1 ndani ya muda mchache.
|