Home
Sign Up
Log In
Wednesday
07.03.2024
7:10 AM
Welcome Guest | RSS

            SALMA SPORTS MEDIA


    PATA HABARI MOTOMOTO ZA MICHEZO NDANI NA NJE YA

NCHI. 

                                                                                                                 TANGAZA NASI



WASILIANA NASI KUPITIA +255 779 518 500 / +255 772 997 018 / +255 678 043 812; email: salmahassan040@gmail.com / salminjsalmin@gmail.com



Site menu

Our poll
Rate my site
Total of answers: 3

Statistics

Total online: 1
Guests: 1
Users: 0

  
Home » 2016 » February » 22 » KAIMU KATIBU MSAIDIZI WA ZFA AFARIKI DUNIA.
8:57 AM
KAIMU KATIBU MSAIDIZI WA ZFA AFARIKI DUNIA.
Mamia ya wananchi na wanamichezo visiwani Pemba jana walikishiriki katika mazishi ya aliyewa kuwa Kaimu katibu Msaidizi wa ZFA Taifa Pemba Marehemu Abdalla Suleiman Sharrif aliyefariki dunia ghafla juzi majira ya saaa saba za mchana.
 
Mazishi hayo yaliyofanyika huko kijijini kwao Mpakanjia yalitanguliwa na ibada ya sala ambayo kabla ilikuwa ifanyike katika uwanja wa mpira wa Uwond\we hata hivyo kutokana na hali ya hewa ya mawingu ililazimika ibada hiyo ifanyike katika msikiti wa Uwondwe.
 
Akizungumzia msiba huo Mjumbe wa Kamati tendaji wa ZFA Wilaya ya Chake Chake Jongo Juma Jongo alisema msiba wa Mw. Abdalla umeacha Pengo katika sekta ya michezo hapa visiwani Pemba kwa vile alikuwa mtu mwenye bidii katika kuona mpira wa miguu unakuwa kisiwani Pemba na Zanzibar kwa ujumla.
 
Naye aliyekuwa katibu wa timu ya "Duma" iliyokuwa ikimilikiwa na JKU Pemba Salum Abdalla alisema kifo cha Maalim Abdalla kimeacha simazi kwao kama wanamichezo na kusema hawakuwa na njia ya kuzuia maamuzi ya Mwenyezimungu na kuwaomba wanafamia ya michezo kumuombea mwenzao ambaye ametangulia mbele ya haki.
 
Kwa upande wake Mwenyekiti wa ZFA Wilaya ya Wete Ali Khamis Mselem amesema hadi anafariki dunia Maalim Abdalla alikuwa ni mwakilishi wao Taifa alisema amewaachia pengo na huzuni kubwa kwa vile ZFA Wilaya ya Wete walikuwa wakimtegemea kwa mambo mengi hasa ya kisheria.
 
Marehemu Abdalla Suleiman Sharrif ambaye kitaaluma ni Mwalimu ameweza kushika nyezifa mbali mbali katika uongozi wa michezo kisiwani Pemba, ikiwemo Kaimu katibu Msaidizi wa ZFA Taifa Pemba, Katibu wa ZFA Wilaya ya Wete, Mjumbe wa Kamati Tendaji wa ZFA Taifa akiiwakilisha Wilaya ya Wete kwa vipindi tofauti, pia alikuwa ni mwalimu wa michezo katika Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali kabla ya kustaafu kazi.
 
Aidha Marehemu Mwalim Abdalla aliwahi kuwa mjumbe wa kamati ya uongozi katika vyama mbali mbali vya michezo visiwani Pemba ikiwemo Chaneza, Baza, ZAVA na Mengineyo.
 
Tunamuomba Mwenyezi Mungu ailaze mahala pema roho ya Marehemu mpendwa wetu Suleiman Abdalla Sharrif na amsamehe makosa yake, Ameen.
Views: 463 | Added by: salminjsalmin | Rating: 0.0/0
Total comments: 0
avatar

Visitors
idadi ya watembeleaji
Idadi ya watembeleaji

WATEMBELEAJI

Entries archive

Salma Sport Media © 2024
uCoz