Home
Sign Up
Log In
Monday
06.23.2025
9:11 AM
Welcome Guest | RSS

            SALMA SPORTS MEDIA


    PATA HABARI MOTOMOTO ZA MICHEZO NDANI NA NJE YA

NCHI. 

                                                                                                                 TANGAZA NASI



WASILIANA NASI KUPITIA +255 779 518 500 / +255 772 997 018 / +255 678 043 812; email: salmahassan040@gmail.com / salminjsalmin@gmail.com



Site menu

Our poll
Rate my site
Total of answers: 3

Statistics

Total online: 1
Guests: 1
Users: 0

  
Home » 2016 » February » 16 » Issa Hamad Mertesacker: Zanzibar itakua juu kisoka kama watatunzwa wenye vipaji
11:19 AM
Issa Hamad Mertesacker: Zanzibar itakua juu kisoka kama watatunzwa wenye vipaji
Kutokana na utafiti maalum niliyoufanya kanda ya unguja (mjini) na baadhi ya mashamba kwa mtazamo wa harakaharaka nimefanikisha kujua kuwa Zanzibar kuna vipaji vingi na vikubwa lakini tatizo liliyopo ni uhaba wa juhudi za kuviendeleza na kuvitunza.
 
Wapo wachezaji wengi ambao wanalisakata kabumbu tena wanavipaji vikubwa hapa nchini lakini mpaka leo hii utashangaa ukiwaona wapo mitaani pasi na kua katika hadhi sawa na vipaji vyao.
 
Katika tafiti hii niligundua vijana wengi sana akiwamo Issa Hamad Mertesacker ambae ni moingoni mwa vijana wanaolisakata kabumbu katika ligi ya vyuo hapa visiwani Zanzibar inayojulikana kwa jina la ZAHILFE CUP wapo tu na wameshakata tamaa.
 
Mertesacker anacheza mpira katika chuo kikuu cha Zanzibar Zanzibar University (ZU) umri miaka ishirini na moja (21) amekuwa akishiriki ligi za vyuo za ndani na nje kwa muda mrefu sasa.
Katika mlolongo wa ligi ni mashindano mengi aliyowahi kushiriki moja ni ya East Africa University Games yaliyofanyika nchini Uganda.
 
Mertesacker ni beki namba mbili anaevalia jezi nambari kumi na tatu mgongoni (13) katika game zake nyingi amekuwa ni tishio kwa timu pinzani.
 
Mertesacker ana uwezo mkubwa wa kuisaidia timu yake pindi inapocheza na sifa yake kuu ni kutengeza nafasi nyingi za kushinda aidha yeye mwenyewe au mwenzake na kwa uthibitisho wa hilo yeye mwenyewe tayari ameshafunga magoli nane (8) katika mechi 25 alizozicheza.
 
Baada ya kukaa nae na kuzungumza mambo mbalimbali katika soka chini alinielezea malengo yake ambayo ameyapanga kuyafikia, moja kati ya hayo anatamani kufika katika kikosi cha timu ya Taifa ya Zanzibar na baadae ajuulikane zadi na dunia nzima na kipaji hicho anacho lakini changamoto anayokabiliana nayo mpaka sasa wadau wanashindwa kujitokeza na kuthamini kipaji chake.
 
Mara baada ya maongezi hayo SALMA SPORTS MEDIA iliamua kujiridhishwa kwa kuona vipi anavyolisakata kabumbu hilo!! ilikua ni katika uwanja wa “Chuo kikuu” (Tunguu) kweli MEDIA hii imeridhika na kipaji chake, ni mchezaji kweli.
 
Unadhani ipo haja ya kuzitoa pesa zetu na kuzipeleka nje ya nchi kwa ajili ya kwenda kuvitafuta vipaji na hali ya kuwa tunavidumaza wenyewe?
Views: 202 | Added by: salminjsalmin | Rating: 0.0/0
Total comments: 0
avatar

Visitors
idadi ya watembeleaji
Idadi ya watembeleaji

WATEMBELEAJI

Entries archive

Salma Sport Media © 2025
uCoz