Sasa Ipo haja kubwa ya kuzitazama na kuzisaidia timu ndogondogo za vijana kama Central, Juvenile na nyenginezo kwani kuna vipaji vya mfano ambavyo kama vitatunzwa hapo baadae tutazalisha wenyewe Akina Ronaldo, Zizu, Mesi, Maradona na wengine.
Wadau wengi sasa wamekua wakielekeza fikra zao na misaada yao katika timu kubwakubwa na kusahau upande wapili wakati ndiko kwenye vyanzo vya kutoa hao wanaoonekana leo ndio bora zaidi..
Kwa ushahidi wa hayo hebu mtazame mtoto Samir Abdallah ni kijana mwenye umri 17, anasakata kabumbu katika klabu ya Small Brazil ya Bububu Zanziabr ngazi ya Central wilaya ya mjini Magharib.
Ni streika hatari sana anaevalia jezi namba 8 mgongoni, ambae mpaka sasa tayari ameshafunga mabao 9 katika michezo saba(7) aliyocheza.
Akiwa uwanjani,hachezi na nyavu,mkakamavu,mweledi,na mzuri wa kufikiria anapofanya maamuzi uwanjwa,hawezi kupoteza pasi uwanjani kikawaida.
Kijana huyu ana ndoto nyingi na nzuri katika maisha yake ya kuweza kufika mbali katika soka lakini wapi,jiulize ni wangapi wenye lengo kama la huyu? leo wako wapi,hakuna wadau wanao watazama wachezaji kama hawa wenye vipaji vya hali ya juu unafikiri Tanzania yetu itaendelea bila ya kuwapa nguvu watoto kama hawa.
Wadau na wahisiani wa soka nchini tazameni hali ya kijana huyu ni hodari wa kweli,timizeni kiu yake yeye na wengineo kwa maendeleo ya soka nchini mwetu,kwa mawasiliano ya kumpata kijana huyu wasiliana kupitia + 255773220869