
Na Abdullatif Omar Famau.
Naam kabla hatujaona kitu gani kilijiri katika mkutano mkuu kwanza tuangalie matukio kadhaa ambayo nimeyaambatanisha na picha hizo hapo chini. Baada ya Coast Asili kufanyiwa hila nyingi za kunyimwa card na viongozi kuwatumia baadhi ya mashabiki na wanachama wao wapya kupinga wengine wasipewe card, kundi la coast Asili lilianza mikakati ya kuusakama uongozi juu ya utendaji wake pia kundi hili lilijenga upinzani mkubwa ndani ya club hii liliamua kuanzisha maskani mpya ya uwanjani pindi club ikicheza.

Kawaida coastal union ikicheza mashabiki wake hukaa jukwaa la kushoto maarufu chuo cha afya, lkn kutokana na kubaguliwa kwake kundi liliamuaa kuanza kukaa upande wa Russia(rasha) na kupiga ngoma huku wakishangilia timu yao sambamba na Banners (mabango) yao makubwa yakiukosoa uongozi na kudai kadi za uanachama... Nakumbuka mabango hayo yaliandikwa hivi:
1. Coastal Asili suporters
2. Uongozi umefeli
3. Mwenyekiti fanya kazi na wajumbe Sio wapambe
4. Kadi za uanachama ni haki yetu.
Mabango hayo yalikuwa yakiwekwa uwanjani kila mechi ya nyumbani ya coastal union, kwakweli uongozi wa coastal union ukiongozwa na mwenyekiti kipindi hicho bwana Hemed Aurora ulichukizwa sana na mabango yale lakini hawakuwa na la kufanya zaidi ya kuyaangalia tu Katika kujitenga huko kwa kundi hili kufanya maskani yake upande wa Russia tulikuwa na sare maalum ambazo zilikuwa na nembo ya muhisani aliyekuwa na ugomvi na uongozi, tulivalia jezi za sound zenye nembo ya Binslum pia...lkn wakati huohuo Coastal union ilikuwa haitumii tena nembo hiyo bali ilipata udhamini mpya kutoka kwa kampuni ya PEMBE FLOUR MILLS na TSN pembe ilivaliwa kifuani na Tsn ilivaliwa chini ya mgongo.

Hivyo chuki ya uongozi kwa kundi hili la coast asili ilikuwa ni zaidi ya mara mbili kwanza, tunadai card za uanachama, pili tunataka uongozi ujirekebishe tatu tulikuwa tunatumia fulana za muhisani asiyetakiwa ilhali club imepata wadhamini wapya. Hali hiyo iliendelea kwa mechi kadhaa mpaka mambo yakawa makubwa kuhusu jezi.
Siku moja tulikuwa na mechi sikumbuki tulikuwa tunacheza ma timu gani lakini ilikuwa ni siku ya jumamosi, tumeshajipanga kuingia uwanjani kama kawaida tukaanza kusambaza jezi zetu za Binslum kumbe, wafuasi wa viongozi pamoja na viongozi hawafurahishwi na kitendo kile cha sisi kuvaa jezi hizo, basi aliyekuwa Team manager Bwana Akida Machai aliongoza operation ya kutafuta watu wenye jezi za Binslum na kuwakamata na kuwapeleka polisi kwa madai ya kutumia nembo isiyo halali kwa club.
Nakumbuka tulishikwa watu wanne na mimi nikiwa mmojawapo, tulipelekwa polisi lakini nakumbuka kwa msaada wa Aliyekuwa makamu mwenyekiti Bwana Steven Mnguto na baba yangu mzazi bwana Omar Abubakar Famau walikuja polisi haraka wakatuchomoa na tukaelekea kuangalia mpira, hata sikumbuki tulifungwa au tulishinda.... Kwanini nimehadithia yote hayo? Najaribu kukuonyesha wewe msomaji ni wapi chuki ilitokea baina ya kundi la coastal Asili na viongozi na kitu gani kilikuwa kinatetewa na coast asili na ni yapi yalikuwa madai ya coast Asili?
Mambo ya ugomvi hayakuishia hapo, watu ambao ni marafiki na ndugu pia waligombana sababu ya mapenzi ya viongozi na wengine wakimpenda muhisani...facebook ilivuma kwa matusi ya upande huu na upande ule mpaka kufikia watu kupelekana polisi na mahakamani kwa ajili ya kutukanana kwenye motandao.
Na mengi zaidi yalitokea mitaani. Kumbuka bado kadi hatujapata, wala mkutano mkuu wa mwaka haujakaliwa, lakini tayari kuna makundi mawili makubwa nayo ni COAST Asili na lile linalounga mkono uongozi, bila ya kusahau makundi haya yanayounga mkono uongozo ni Coast nyumba~ hawa walikuwa wako karibu kabisa na club jengine ni mnarani hawa maskani yao ni ile roundabout ya mabanda ya papa na jengine linaitwa makorora hili maskani yake ni Huko makorora lilikuwa likiongozwa na bwana Nassor kibabed.
Nisichoke kukukumbusha ndugu msomaji makundi yote haya hayakuwepo hapo awali bali yalianza kutengenezwa na kupewa card kwa ajili tu ya kulipinga kundi la coast asili na mipango ya mapema ya uchaguzi. Chini hapa nimekuletea picha zikionyesha mabango ya coast asili pia picha nyingine ikionyesha mmiliki wa kampuni ya Binslum tyres akipinga kitendo cha polisi kuwashika mashabiki sababu ya kuvaa jezi zake....
Itaendelea
|