Na Abdullatif Omar Famau.
Kama tulivyoona sehemu ya kwanza kundi la coast Asili limeanza harakati za kudai kadi za uanachama na uongozi unakataa kutoa kadi kwa sababu zisomsingi huku wakigawa kadi kwa watu wengine hata sio wapenzi wa coast...
Jambo hili kwakweli lilianza kuutafuna umoja wa Coastal union, sina hakika kama uongozi ulikuwa unajua nini unachokifanya na zipi zitakuwa ni athari zake kwa kuwagawa wanachama na wapenzi kuwa katika makundi mawili tofauti moja likitaka kuingia ndani ya club na jengine likifundishwa kuwazuia wenzao wasiingie kwa club kihalali.

Ndugu msomaji ukumbuke hili kundi la coast Asili lilijaa vijana wengi na wazee wengi wa mjini, na hawakuona sababu ya kuwa na kadi za uanachama hapo awali wakiamini wao ni wapenzi wa dhati wa coastal tangu wazee wao na hata wao wenyewe. Hivyo walilazimika kuwa na kadi kutokana na mfumo wa kisasa na ubaguzi uliojitokeza...hapa sasa kundi la coast asili likaanza kuimarika kwa kufanya mikutano ya siri ya kupanga mikakati, kufungua ofisi yao ambayo ilijulikana kama COAST ASILI SOCIAL CLUB nayo ilikuwa jirani kabisa na makao makuu ya club yenyewe. na mwisho kundi likapata wanachama wengi zaidi ya 300 wote wakitaka kadi za coastal union.
Coast Asili walianza na kuandika barua ya wazi kwenda kwa katibu wa Club ya Coastal union, barua ambayo ilichapishwa magazetini na kusomwa maredioni pia Televisheni kadhaa kuonyesha jambo hili...uongozi wa coastal inion kupitia mwenyekiti ulipoulizwa jambo hili walikana kuwanyima kadi wapenzi hao bali walisema utatoa kadi hapo baadae kwani kwa sasa club ina mambo mengi ya msingi ya kufanya na sio kadi.
Vuta nikuvute iliendelea kwa takribani miezi kadhaa...mpaka hapo TFF ilipoliingilia jambo hili kati na kumtuma mwanasheria wake bwana Eliud mvela kujua ni nini kinachoendelea Coastal union? Haraka uongozi ukapewa Amri ya kuweka milango wazi kwa mpenzi atakae kupewa form ya uanachama na kusubiri kujadiliwa kwenye mkutano mkuu.. Uongozi wa Coastal union ulitii amri hiyo lakini cha kushangaza form zilikuwa zinauzwa sh 1000 zikapandishwa bei mpaka sh 10,000. Ili kuwafanya Coast Asili washindwe kununua form, lakini huku mitaani ukipita unaona kuna watu wana card za coastal union tena mpya...ukiwauliza wanasema wamepewa bure na wengine wamelipia sh 5000 hawakujaza form wala kujadiliwa na mkutano mkuu wa wanachama kama katiba inavyosema.
Coast Asili iliwanuia vigumu kununua form kwa sh 10000 lkn kupitia wahisani wake iliweza kupatikana fedha zaidi ya mil 1.5 kununua form zaidi ya 150 na wengine waliojiweza walinunua kwa pesa zao...lkn sasa tayari ikawa ndani ya coast kuna makundi mawili makubwa moja linaunga mkono uongozi na jengine ndio hili linalojiita Coast Asili likiwa na imani na yule mhisani (mmiliki wa kampuni ya BINSLUM) pia likitetea kupata kadi ili waje kuchagua viongozi wazuri ambao watafanya kazi na muhisani huyo.
Baada ya manunuzi ya form za uanachama kawaida form zilirudishwa kwa katibu wa club bwana kassim El siagi tukisubiri kujadiliwa katika mkutano mkuu ili tujue hatma yetu.. Je tutakuwa wanachama au la?
Usikose kusoma kesho Insha Allah uone nini kilitokea katika mkutano mkuu wa wanachama....
|