
Na Abdullatif Omar Famau.
Najaribu kuandika makala haya lengo ni kuwafungua masikio watu wengi ambao hawajui sintofahamu ya Coastal union. Pia naamini nina mengi nayafahamu kwanini coast haifanyi vizuri. Nitajaribu kuandika bila ya kumtaja mtu jina wala kumkosea mtu adabu. Hivyo pia ukijaaliwa ku-comment usinikosee adabu.
Coastal union ni club kongwe ya nne nchini Tanzania ikitanguliwa na Yanga, Simba na sports. Yanga na simba zimekuwa zikionekana kufanya vizuri japo mimi nasema bado kwani wanatakiwa kuwa zaidi ya Azam. Watani zenu African sports nitawaekea jiwe.
Coastal imemaliza kuwa timu bora mwishoni mwa miaka 80 kwa kutwaa ubingwa wa bara mwaka 88 na ilipoanza miaka ya 90 haikuwa tena timu ya kusifika pia ilikuwa ikishuka daraja na kupanda. Ilipanda tena kuwa ligi kuu mnamo 2010 pia kulifanyika uchaguzi wa mwenyekiti na wajumbe wake ambao tunaweza kusema si uchaguzi wa vuta nikuvute kwani aliyesimama nafasi ya mwenyekiti alikuwa mtu mmoja na wanachama wote waliridhia kumpa kura kwa kutambua umuhimu wake katika kuisimamia timu kupanda ligi kuu. Kipindi hicho coastal union ilikuwa na wanachamd hai sio zaidi ya 70 na wote walikuwa coastal union tu.
Ilipoanza ligi bado wanachama na washabiki walikuwa kitu kimoja na baadae kukatokea sintofahamu ya muhisani wa coastal union na uongozi wa club kuhusu matumizi ya kuweka nembo ya muhisani bila ya malipo kwa club na muhisani nae akidai kuwa anaisaidi club. Mambo haya yalichukua nafasi kubwa sana katika vyombo vya habari, pia yalitenganisha ule umoja wa wana coastal wengine wakimuunga mkono muhisani na wengine wakaunga mkono uongozi. Hali hii ikasababisha kuundwa kwa kundi la coast asili ambalo lilikuwa na imani kubwa ya muhisani na kuanzisha mapambano ya kumtetea muhisani. Uongozi nao haukuwa umelala ulijiimarisha ipasavyo kuhakisha wanatetea wanachokiamini. Kundi la COAST ASILI likaanza na harakati za madai ya kadi ya uanachama wakiamini wakiwa wanachama watakuwa na uwezo wa kupiga kura na kushiriki mikutano ya coast na kufanya maamuzi. Uongozi nao ukaamua kutumia nguvu zake kuwafanyia hila kundi la coast Asili kuwanyima card za uanachama wakiamini kwamba hawa wakiwa wengi wataweza kufanya maamuzi na hata kupiga kura kuweka viongozi wanaowataka lakini hapohapo uongozi unafanya dhambi ya kugawa kadi za uanachama bure kwa watu wawatakao na kufungua matawi na kuyapa vyeti hii ni kuhakikisha uongozi nao unakuwa na kundi kubwa la wanachama ambalo watalitumia katika mikutano na hata uchaguzi....
Itaendelea
|