Timu ya Chelsea ilitoana jasho na Newcastle United katika mechi ya wiki ya 26 ya EPLiliyochezwa katika uwanja wa Stamford Bridge.
Chelsea yaondoka na pointi 3 baada ya ushindi mnene dhidi ya Newcastle United

Chelsea iliyoanza kwa kishindo iliweza kuleta faraja kwa mashabiki wake na kuondoka na pointi 3 baada ya kuicharaza Newcastle United bao 5-1.
Magoli ya Chelsea yalifungwa na Costa (dakika ya 5), Pedro (dakika ya 9 na 59), Willian ( dakika ya 17) na Traore (dakika ya 83).
Newcastle United nao walipata goli la futia machozi kupitia Townsend aliyefunga katika dakika ya 90.
|