Home
Sign Up
Log In
Monday
06.23.2025
9:17 AM
Welcome Guest | RSS

            SALMA SPORTS MEDIA


    PATA HABARI MOTOMOTO ZA MICHEZO NDANI NA NJE YA

NCHI. 

                                                                                                                 TANGAZA NASI



WASILIANA NASI KUPITIA +255 779 518 500 / +255 772 997 018 / +255 678 043 812; email: salmahassan040@gmail.com / salminjsalmin@gmail.com



Site menu

Our poll
Rate my site
Total of answers: 3

Statistics

Total online: 1
Guests: 1
Users: 0

  
Home » 2016 » February » 20 » Blatter: simuungi mkono mgombea yeyote
7:32 PM
Blatter: simuungi mkono mgombea yeyote

Sepp Blatter amesema hatomuunga mkono yeyote kati ya wagombea watano wanaosimama katika uchaguzi wa kumrithi kama rais wa FIFA, japokuwa wote isipokuwa mmoa wamezungumza naye kuhusu maombi yao

Shirikisho hilo la kandanda ulimwenguni ambalo limegubikwa na kashfa ya rushwa ambayo ilisababisha maafisa kadhaa wakuu kufunguliwa mashtaka nchini Marekani, litaandaa uchaguzi wa kumpata kiongozi wake mpya mnamo Februari 26. Blater hatogombea, baada ya kupigwa marufuku kwa miaka minane kwa ukiukaji wa maadili.

Na sasa Mswisi huyo anasema wagombea watano wamezungumza naye, lakini hawezi kuegea upande wowote, maana hilo haliwezekani. Aidha amesema mashirika kadhaa ya kitaifa yamemuuliza nani yanapaswa kumpigia kura, lakini akayaambia yapige kura kutokana na uamuzi wao. Blatter anasikitika kuwa vyombo vya habari vilimwangamiza "ninachojutia ni jinsi vyombo vya habari vilivyoamua kuniuwa kuanzia siku ya kwanza. shutuma dhidi ya rais wa FIFA kutoka kwa vyombo vya habari wakati sikuwa mwenye anayewajibikia hatua za wanachama wa Kamati Kuu kwa vile sio mimi ninayewachagua. majuto yangu ni kuwa, labda, kuwa hatuchukua hatua mwafaka ili kuepuka kuwa na wanachama wa kamati kuu ya FIFA ambao hawakupita mtihani wa uadilifu".

Wagombea wakuu wawili ni Sheikh Salman bin Ebrahim al-Khalifa wa Bahrain na Katibu Mkuu wa UEFA Gianni Infantino wa Uswisi. Wengine ni Mwanamfalme wa Jordan Ali bin al-Hussein, Mfaransa Jerome Champagne, naibu katibu mkuu wa zamani wa FIFA, na mfanyabiashara wa Afrika Kusini na mwanasiasa Tokyo Sexwale.

Views: 205 | Added by: salminjsalmin | Rating: 0.0/0
Total comments: 0
avatar

Visitors
idadi ya watembeleaji
Idadi ya watembeleaji

WATEMBELEAJI

Entries archive

Salma Sport Media © 2025
uCoz