Home
Sign Up
Log In
Monday
06.23.2025
10:27 AM
Welcome Guest | RSS

            SALMA SPORTS MEDIA


    PATA HABARI MOTOMOTO ZA MICHEZO NDANI NA NJE YA

NCHI. 

                                                                                                                 TANGAZA NASI



WASILIANA NASI KUPITIA +255 779 518 500 / +255 772 997 018 / +255 678 043 812; email: salmahassan040@gmail.com / salminjsalmin@gmail.com



Site menu

Our poll
Rate my site
Total of answers: 3

Statistics

Total online: 1
Guests: 1
Users: 0

  
Home » 2016 » February » 16 » BLACK SAILORS WAKABWA KOO NA POLISI.
10:55 PM
BLACK SAILORS WAKABWA KOO NA POLISI.

Mara baada ya majigambo ya msemaji wa Black sailors ya kusema kuwa watashinda katika mechi yao kati ya Polisi hatimae wakubali kutoka sare katika mchezo huo.

 

Timu ya Black sailors na Polisi leo zimeshindwa kutambiana katika mchezo wa muendelezo wa ligi kuu ya Zanzibar kanda ya Unguja,baada ya kutoka sare ya bila kufungana.Katika mchezo huo timu zote zilionekana kutafuta alama tatu muhimu katka ligi hiyo.

Black sailors iliyovalia jezi rangi nyeusi na Polisi imevalia jezi rangi nyeupe.

Kocha wa timu ya kikosi cha Polisi Ali Suleiman Mtuli amesema kuwa, hawakutakiwa kutoka sare katika mchezo huo ila  walitakiwa washinde lakini ameongeza kwa kusema kuwa bado kuna matatizo katika  kikosi chake hivyo wanatakiwa wayatatue ili waweze kujinasua katika kushuka daraja.

 Aidha kwa upande wake kocha wa black sailors amesema Juma Awadh,amesema waliweza kupata nafasi za kufunga lakini nafasi hizo timu yake imeshindwa kuzitumia vizuri, lakini ndo mpira kwani bahati haikuwa ya kwao na wao wameyakubali matokeo hayo.

Timu ya Polisi ambayo bado inaonekana kusuasua katika ligi kuu ya Zanzibar  imeshacheza michezo kumi na nne (14) wakiwa nafasi ya  kumi na tatu 13 na alama na 8, huku Black sailor wao wakiwa na alama (22) wakishika nafasi ya nne (4).

Huu ni mzunguko wa pili katika ligi kuu ambao ni wa lala salama ambapo mzunguko wa mwanzo timu hizi zilipokutana Black sailors walifanikiwa kuwafunga maafande hao wa Polisi.

Views: 148 | Added by: salminjsalmin | Rating: 0.0/0
Total comments: 0
avatar

Visitors
idadi ya watembeleaji
Idadi ya watembeleaji

WATEMBELEAJI

Entries archive

Salma Sport Media © 2025
uCoz