Timu ya Liverpool ilipambana na Aston Villa kwenye mechi ya wiki ya 26 ya ligi kuu ya soka ya EPL nchini Uingereza.
Liverpool yaondoka na pointi 3 ugenini baada ya kuinyeshea Aston Villa mvua ya magoli
Aston Villa ambayo inatapatapa kwenye jedwali la EPL, ilishindwa kujinasua mkiani baada ya kucharazwa na Liverpool bao 6 bila jibu.
Magoli ya Liverpool yalifungwa na Sturridge (dk. 16), Milner (dk. 25), Emre Can (dk. 58), Origi (dk. 63), Clyne (dk. 65) na Toure (dk. 71).
Ushindi huo mnene umewezesha Liverpool kupanda hadi nafasi ya 8 ikiwa na pointi 38.
|