Chama cha Mpira wa Miguu Zanzibar (ZFA) na wadau wengine mbalimbali nchini wametakiwa kuongeza juhudi zaidi katika kuhakikisha wanaendeleza ligi na mashindano ya michezo tofauti ili kuibua vipaji vya wanamichezo, hatua hiyo itasaidia pakubwa kwa taifa kujizalishia vipaji vyake wenyewe badala ya timu kutegemea wachezaji wazuri kutoka nje.
Hayo yameelezwa na kiungo wa timu ya KVZ Suleiman AbdiMuller wakati alipokuwa akizungumza na mwanamichezo wako kutoka SALMA SPORT MEDIA juu ya maendeleo na changamoto za soka nchini Zanzibar.
Muller ni mchezaji machachari sana akiwepo kiwanjani,ni mchezaji anaebeba nambari kumi na tatu (13) mgongoni katika timu ya KVZ, pia ni mchezaji anaekubalika sana kwa wadau wa soka hasa katika kukaba kwenye nafasi ya midfield na asiye yumba katika maamuzi yake wakati anapolisakata kabumbu,hakika wachezaji kama hawa ndio wakuenziwa na kuhifadhiwa vizuri.
Tulizungumza mengi sana katika soka letu nchini ZanzIbar na maongezi yetu yalikua kama ifuatavyo:-
Salma Sports Media: Wewe ni mdau mkubwa wa soka letu hapa Zanzibar, je, kiupande wako unalionaje?
Muller: Soka lipo zenji tena lipo la kiwango cha hali ya juu ila vipaji tunavidumaza wenyewe kwa mambo tofauti ikiwamo “siasa” hili ni tatizo sugu ndio imetawala visiwani mwetu, lakini pia hatuelewi kwa upande wa Pemba ligi haichezwi unadhani tunategemea nini mwishoni salma!!
Salma Sports Media: Sasa kama hali ndio hivyo unaushauri gani au nini kifanyike ili kuondokana na haya ili viwango vyetu vizidi kukua nchini.
Muller: Nahis tuwekeze sana kwenye michezo na tuangalie sana vipaji hasahasa kwa watoto wa madaraja ya chini tuwatunze ili baadae tupate wachezaj wazuri Zaidi na ligi zichezwe kwa wakati ili timu zipate kuwa fit.
Salma Sports Media: Imekua ikisikika tu kwa wadau kwamba una kipaji na uwezo mzuri wa kucheza soka, unaweza kuwathibitishia wadau watakaosoma habari hii juu ya uwezo wako mwenyewe ni sawa na wanavyosema na kukusifia au unalizungumziaji hili?
Muller: Hahahahahaaa!! kiukweli pengine hawajakosea ila ninavyojijua mimi ni kua nina uwezo wa kuchezesha timu na kukaba kwenye nafasi ya midfield maana makocha wengi wanavutiwa na kiwango changu na wanatamani siku moja nicheze kwenye club zao.
Salma Sports Media: na unamalengo gani umepanga kuyafikia katika uchezaji wako?
Muller:Malengo ninayo makubwa tu ni kufika mbali na kucheza njee ya nchi lakini hata hapa nchini natamani kucheza hata vilabu vya apo bongo kam Simba , Yanga na Azam lakini kubwa Zaidi ni kuiwakilisha nchi yangu nje katika mataifa makubwa na naamini ipo siku nitafanikiwa kutokana na juhudi ninayoichukua,na nadhani hii inaonekana wazi kabisa na washabiki pamoja na wadau wanaoniona nikiwa kiwanjani.
SalmaSport Media: Unawambia nini wadau wa soka nchini kwa ujumal?
Muller: Nawaomba tu nguvu zao kuzielekeza kwa wachezaji hasa wadogo kuwainua,maana ukweli huko chini ndio kwenye vipaji vya hali ya juu lakini pia wadau wangu kwa ujumla nawaomba waniombee dua na nawaahidi nitawafanyia vitu vizuri watazidi kunipenda na hata wasio nipenda lazima tu watavutiwa na mimi.
Muller ni mchezaji wa KVZ inayocheza ligi kuu ya Zanzibar kanda ya Unguja.
|