Home
Sign Up
Log In
Wednesday
07.03.2024
7:07 AM
Welcome Guest | RSS

            SALMA SPORTS MEDIA


    PATA HABARI MOTOMOTO ZA MICHEZO NDANI NA NJE YA

NCHI. 

                                                                                                                 TANGAZA NASI



WASILIANA NASI KUPITIA +255 779 518 500 / +255 772 997 018 / +255 678 043 812; email: salmahassan040@gmail.com / salminjsalmin@gmail.com



Site menu

Our poll
Rate my site
Total of answers: 3

Statistics

Total online: 1
Guests: 1
Users: 0

  
Home » 2016 » February » 23 » SALMA OMAR NI MMOJA KATI YA WACHEZAJI JUDO ZANZIBAR WALIOONDOKA KWENDA KATIKA MAPAMBANO
6:11 AM
SALMA OMAR NI MMOJA KATI YA WACHEZAJI JUDO ZANZIBAR WALIOONDOKA KWENDA KATIKA MAPAMBANO
Msafara wa watu 17 wa mchezo wa Judo Zanzibar umeondoka visiwani Zanzibar mchana wa jana na kuelekea Tanzania bara ambapo leo moja kwa moja wataanza kwenda mjini Bunjubura nchini Burundi katika mashindano ya Afrika Mashariki ya mchezo huo wa Judo.
 
Mashindano hayo yanatarajiwa kufanyika tarehe 26-27 ya mwezi huu wa Februari kwa nchi mbali mbali za Afrika Mashariki.
 
Raisi wa Heshima wa mchezo huo wa judo Zanzibar mwenye asili ya Japani Abdul Halim Shimaoka amesema wao kama Zanzibar wamejiandaa vizuri licha ya vikwazo mbali mbali walivyokumbana navyo ikiwemo mambo vya Siasa lakini anaamini vijana wake watarudi na ubingwa ambapo pia akijivunia wachezaji wake watatu waliopata mafunzo nchini Japani hivi karibuni.
 
Kwa upande wake mchezaji Salma Omar ambae anacheza mchezo huo kiwango cha uzito wa kilo 52 ambapo pia ni mwanamke pekee mwaka huu kutoka Zanzibar kwenda katika Mashindano hayo huko Burundi anaelezea jinsi gani alivojiandaa katika mashindano hayo ambapo amesema ana ndoto za kuwa mchezaji bora wa mashindano ya Jumuiya za Madola, hivyo lazima apigane ki kike ili aoneshe kama yeye ni mwanamke shujaa kutoka visiwani Zanzibar na anaajiamini atafanya vizuri.
 
Mbali ya hayo lakini matumaini yake ni kutwaa ubingwa kwa asilimia kubwa kwa yule atakae pangwa nae.
 
Katika mashindano hayo Zanzibar imepeleka wawakilishi wao watakaoshindana ambao wana uzito tofauti wakiwemo Azan Hussein na Ali Juma wao watashiriki Judo kwa Uzito wa kilo 60.
Abdul rabi Alawi na Mansabu Alawi ni ndugu hao watacheza Judo kwa wenye Uzito wa kilo 66.
 
Kwa upande wa uzito wa kilo 73 yupo Hafidh Makame pekee ambapo kwa uzito wa kilo 81 atawakilisha Mbarouk Suleiman, wakati huo huo huo Rajab Kassim atashiriki kwa wenye uzito wa kilo 90 na Masoud Amour yeye atashiriki uzito wa kilo 100, Mohd Abdul-rahman na Iddi Othman watashindana uzito wa zaidi ya kilo 100.
 
Hao ndio wawakilishi wa Zanzibar katika mashindano ya 10 ya JUDO ya Afrika mashariki ambayo yatafanyika Burundi tarehe 26-27 ya mwezi huu wa pili ambapo mkuu wa msafara huo ni Yussuf Thabit akikamilisha idadi ya watu 17 wakiwemo wachezaji pamoja na viongozi.
Views: 314 | Added by: salminjsalmin | Rating: 0.0/0
Total comments: 0
avatar

Visitors
idadi ya watembeleaji
Idadi ya watembeleaji

WATEMBELEAJI

Entries archive

Salma Sport Media © 2024
uCoz