Home
Sign Up
Log In
Wednesday
07.03.2024
6:24 AM
Welcome Guest | RSS

            SALMA SPORTS MEDIA


    PATA HABARI MOTOMOTO ZA MICHEZO NDANI NA NJE YA

NCHI. 

                                                                                                                 TANGAZA NASI



WASILIANA NASI KUPITIA +255 779 518 500 / +255 772 997 018 / +255 678 043 812; email: salmahassan040@gmail.com / salminjsalmin@gmail.com



Site menu

Our poll
Rate my site
Total of answers: 3

Statistics

Total online: 1
Guests: 1
Users: 0

  
Home » 2016 » February » 23 » JANG’OMBE BOYS VS KIPANGA, BLACK SAILORS VS JKU, NANI ZAIDI?
9:48 AM
JANG’OMBE BOYS VS KIPANGA, BLACK SAILORS VS JKU, NANI ZAIDI?

 

Usikose kuangalia mitanange ya kukata na shoka leo hii kwa kuchezwa michezo miwili ya muendelezo wa ligi kuu ya Zanzibar kanda ya Unguja ndani ya dimba la Amani, ambapo saa kumi za jioni Jang’ombe boys watavaana na Kipanga na majira ya saa kumi na mbili 12 za jioni, Black sailors watachuana na JKU.

Jang’ombe wameshacheza mechi kumi na tatu (13), waataingia dimbani wakiwa nafasi ya kumi (10) na alama (16), huku wakiw...a wameshinda michezo minne (4), wamepoteza mitano (5) na sare michezo minne (4), na wapinzani wao Kipanga wao wapo nafasi ya kumi na moja (11), wamecheza mechi kumi na nne (14), wameshinda mitatu (3), wamepoteza michezo minne (4), michezo saba (7) wametoka sare na wana alama kumi na sita (16).

Kwa upande wa JKU wao wakiwa ndio kinara wa ligi hiyo wataingia uwanjani wakiwa na alama (32), wamepoteza mchezo mmoja katika michezo kumi na tatu (13) waliyocheza huku wakitoka sare michezo miwili, wakati Black sailors wao wataingia uwanjani wakiwa wamecheza michezo kumi na nne (14), wameshinda michezo sita (6), sare michezo minne (4) na wamepoteza minne (4),wanakamata nafasi ya tano (5) na alama zao ni (23).

Views: 361 | Added by: salminjsalmin | Rating: 0.0/0
Total comments: 0
avatar

Visitors
idadi ya watembeleaji
Idadi ya watembeleaji

WATEMBELEAJI

Entries archive

Salma Sport Media © 2024
uCoz